Tuesday 29 May 2018

JINSI YA KUPATA MKOPO

Shalom vicoba group imekuwa ikitoa mikopo na kusajili wanachama wapya toka mwaka 2016. Shalom vicoba group iliendelea kufanya kazi Kama kikundi cha kukopeshana na kufikia mwaka 2019 mwezi wa nne ilisajiliwa rasmi Kama Saccos.
Saccos hiyo iliitwa shalom saccos Limited na kupata usajili namba SIR/733.
Ili uweze kupata mkopo unao hitaji lazima uwe na vigezo vifuatavyo:-
  1. Uwe umejiunga kwenye shalom vicoba group na kulipia kiingilio cha Tshs. 30,000/=
  2. Uwe umenunua HISA za msingi 20 ambapo kila Hisa huuzwa kwa Tshs 10,000/= na Jumla kupelekea Tshs. 200,000/=
  3. Uwe mtendakazi kwenye makanisa yenye ushirika wenza na shirika la Compassion International Tanzania.
  4. Uwe na mkataba wa kazi wa sasa.
  5. Uwe na AKIBA itakayokuwezesha kukopa mara tatu ya kiwango unachohitaji. Mfano unataka kukopa milioni tatu, basi LAZIMA uwe na AKIBA ya Tshs. 1,000,000/=

VIAMBATANISHO WAKATI WA KUCHUKUA MKOPO.
  1.  Fomu ya mkopo ambayo inapatikana kwa Tshs. 10,000/= tu.
  2. Mkataba wa ajira
  3. salary slip tatu za hivi karibuni zilizosainiwa na mwajiri na kuwekwa Muhuri.
  4. standing order ya Benki

Saturday 26 May 2018

SERA YA UWEKAJI AKIBA, AMANA NA UTOAJI WA MIKOPO (svg)


SEHEMU YA KWANZA.

UTANGULIZI:

Sera ya mikopo ya SVG ni taratibu zilizowekwa na Chama kwa ajili ya kusimamia namna ya utoaji wa mikopo ndani ya chama na ni ramani ya chama inayoonyesha namna ya kutoa mikopo kwa wanachama wake.  Taratibu hizi za mikopo zimetungwa kwa kufikiria misingi ya kanuni za utendaji bora wa taasisi za huduma za kifedha na lazima zifuatwe na zitumike kulingana na sera hii na Bila ya kuathiri sheria za Nchi.
Shalom vicoba group imesajiliwa kwa namba IDC/CSO/613 Rasmi mnamo tarehe 08/12/2017 na Akaunti yake ni 50610009672 Jina la akaunti ni Shalom Group. Mpaka siku ya usajili chama kilikuwa na wajumbe waliojiandikisha jumla ya kumi na saba (17) tu.

1.           MADHUMUNI YA SERA YA MIKOPO

Madhumuni ya sera hii ni kuweka utaratibu wa utoaji mikopo kwa wanachama wa SVG na wadau wengine wa mikopo ambao watakubalika na Bodi ya Uongozi kulingana na wakati. Pia kuweka misingi bora ya usimamizi wa mikopo kwa lengo la kuepuka majanga yatokanayo na mikopo mibaya ndani ya chama.

2.           WALENGWA WA SERA YA MIKOPO

Walengwa wa sera hii ni wale wote watakaokuwa wakihusika na mikopo kwa namna moja ama nyingine ikiwa ni pamoja na waombaji, wapitiaji, waidhinishaji, na wasimamiaji wa mikopo katika SVG; Pamoja na wengine watakaohusika na sera hii kwa namna moja ama nyingine, sera itawahusu moja kwa moja wafuatao: -

(i)            Wanachama binafsi
(ii)         Vikundi vya wanachama
(iii)        Vikundi vinavyotambulika kijamii na vinavyoendeshwa kwa mujibu wa sheria.
     
(iv)        Wateja wengine kwa ridhaa ya mkutano mkuu wa wanachama.
(v)          Wafanyakazi waajiriwa na wastaafu wa SVG.

(a)          Wadau wa ndani

       (i)    Wanachama ndio walengwa wakuu wa Sera hii kwa kuwa ndio wakopaji
                
(ii)     Wafanyakazi/Watendaji – Hawa ni wataalamu wa kuchanganua na kutathmini mikopo inayoombwa na inayotolewa.
(iii)    Viongozi wa SVG ndio wasimamizi wa kuhakikisha kuwa taratibu zote za Sera zinafuatwa


 (b)       Wadau wa nje

(i)       Wakaguzi wa nje – Watatumia Sera hii wakati wa ukaguzi wa fedha na mali za svg hii.

(ii)     Afisa ushirika – Ni mshauri katika utekelezaji wa sera hii kama mwakilishi wa Serikali.

(iii)    Taasisi za ukopeshaji – Chama kitakopa toka taasisi za kifedha kulingana na taratibu za sera hii.

(iv)    Mrajisi wa vyama vya Ushirika – Ndiye anayepitisha sera hii na kuridhia kwa ajili ya kutumika.


Je, Ungependa kupata KATIBA na SERA ya Mikopo?
tuma email ya maombi kwenye: cdwssaccos.tz@gmail.com