SEHEMU
YA KWANZA.
UTANGULIZI:
Sera
ya mikopo ya SVG ni taratibu zilizowekwa na Chama kwa ajili ya kusimamia namna
ya utoaji wa mikopo ndani ya chama na ni ramani ya chama inayoonyesha namna ya
kutoa mikopo kwa wanachama wake. Taratibu
hizi za mikopo zimetungwa kwa kufikiria misingi ya kanuni za utendaji bora wa
taasisi za huduma za kifedha na lazima zifuatwe na zitumike kulingana na sera
hii na Bila ya kuathiri sheria za Nchi.
Shalom
vicoba group imesajiliwa kwa namba IDC/CSO/613
Rasmi
mnamo tarehe 08/12/2017 na Akaunti yake ni 50610009672
Jina la akaunti ni Shalom Group. Mpaka
siku ya usajili chama kilikuwa na wajumbe waliojiandikisha jumla ya kumi na
saba (17) tu.
1.
MADHUMUNI YA SERA YA MIKOPO
Madhumuni
ya sera hii ni kuweka utaratibu wa utoaji mikopo kwa wanachama wa SVG na wadau wengine wa mikopo ambao
watakubalika na Bodi ya Uongozi kulingana na wakati. Pia kuweka misingi bora ya
usimamizi wa mikopo kwa lengo la kuepuka majanga yatokanayo na mikopo mibaya
ndani ya chama.
2.
WALENGWA WA SERA YA MIKOPO
Walengwa
wa sera hii ni wale wote watakaokuwa wakihusika na mikopo kwa namna moja ama
nyingine ikiwa ni pamoja na waombaji, wapitiaji, waidhinishaji, na wasimamiaji
wa mikopo katika SVG; Pamoja na wengine watakaohusika na sera hii kwa namna
moja ama nyingine, sera itawahusu moja kwa moja wafuatao: -
(i)
Wanachama binafsi
(ii)
Vikundi vya wanachama
(iii)
Vikundi vinavyotambulika kijamii na vinavyoendeshwa kwa mujibu wa
sheria.
(iv)
Wateja wengine kwa ridhaa ya mkutano mkuu wa
wanachama.
(v)
Wafanyakazi waajiriwa na wastaafu wa SVG.
(a)
Wadau wa ndani
(i) Wanachama
ndio walengwa wakuu wa Sera hii kwa kuwa ndio wakopaji
(ii) Wafanyakazi/Watendaji – Hawa ni
wataalamu wa kuchanganua na kutathmini mikopo inayoombwa na inayotolewa.
(iii) Viongozi wa SVG ndio wasimamizi
wa kuhakikisha kuwa taratibu zote za Sera zinafuatwa
(b)
Wadau wa nje
(i) Wakaguzi wa nje – Watatumia Sera
hii wakati wa ukaguzi wa fedha na mali za svg hii.
(ii) Afisa ushirika – Ni mshauri
katika utekelezaji wa sera hii kama mwakilishi wa Serikali.
(iii) Taasisi za ukopeshaji – Chama
kitakopa toka taasisi za kifedha kulingana na taratibu za sera hii.
(iv) Mrajisi wa vyama vya Ushirika –
Ndiye anayepitisha sera hii na kuridhia kwa ajili ya kutumika.
Je, Ungependa kupata KATIBA na SERA ya Mikopo?
tuma email ya maombi kwenye: cdwssaccos.tz@gmail.com
No comments:
Post a Comment